GET /api/v0.1/hansard/entries/873884/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 873884,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873884/?format=api",
    "text_counter": 167,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Meru CWR, Independent",
    "speaker_title": "Hon (Ms.) Kawira Mwangaza",
    "speaker": {
        "id": 1325,
        "legal_name": "Kawira Mwangaza Mwenda",
        "slug": "kawira-mwangaza-mwenda"
    },
    "content": "Tukiangalia katika nchi yetu ya Kenya, umaskini unachangia sana magonjwa mengi ambayo yanaumiza watu wetu. Huyu maskini anapoenda kutafuta dawa ama matibabu katika hospitali zetu za umma, na haswa katika hospital za kaunti, anapata hakuna dawa, madaktari ni wachache na huduma ni mbaya. Hivyo basi, inasababisha vifo vingi. Watu wanafariki ama wanapatwa na shida, haswa ya kutoa watu hospitali moja hadi nyingine. Hii ni changamoto kubwa, haswa ada zinapokuwa za juu. Kwa hivyo, ningependa kumuunga mkono Mbunge mwenzagu ya kwamba ni heri Serikali ifutilie mbali ada za matibabu katika hospitali za umma za rufaa pindi mtu anapofariki."
}