GET /api/v0.1/hansard/entries/873905/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 873905,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873905/?format=api",
"text_counter": 188,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kilifi South, ODM",
"speaker_title": "Hon. Ken Chonga",
"speaker": {
"id": 13374,
"legal_name": "Richard Ken Chonga Kiti",
"slug": "richard-ken-chonga-kiti"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika. Nasimama kuunga mkono Hoja hii hata ingawa nafikiria ilikuwa inahitaji kupigwa msasa kiasi. Inazingatia wengi ambao wanakufa katika hospitali za rufaa ama wale ambao wanakufa wakiuguliwa katika hospitali za rufaa. Lakini inahitajika kueleweka ya kwamba wengi ambao wanakufa katika hospitali hizi ni wale ambao hali yao ya kiuchumi ni ya chini ama hafifu. Wengi ni maskini. Wengine hata hawawezi kufika hata kwa hospitali ya rufaa. Wanaenda kwa zahanati kijijini na huenda wakafa huko. Kufa huko, kama tunavyojua, ni lazima kila maiti ifanyiwe upasuaji ili kiini cha kifo kikaguliwe. Kwa hivyo, sio hospitali za rufaa peke yake. Hata zile za chini kama zahanati watu hufa huko na shida inakuwa ni ile ile."
}