GET /api/v0.1/hansard/entries/873906/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 873906,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873906/?format=api",
"text_counter": 189,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kilifi South, ODM",
"speaker_title": "Hon. Ken Chonga",
"speaker": {
"id": 13374,
"legal_name": "Richard Ken Chonga Kiti",
"slug": "richard-ken-chonga-kiti"
},
"content": "Nasisitiza ya kwamba wenye tunajua wanakufa kwa hospitali za umma ni maskini, wale ambao hali zao ni duni. Kuna sababu nyingi mbali na zile ambazo Mhe. Mohamed Ali amezitaja. Kuna wale ambao wanakufa wakilala nyumbani. Akipelekwa hospitali, inasemekana lazima kwanza afanyiwe upasuaji. Kwa wale ambao hawaelewi, inaitwa postmortem. Kuna wengine pengine wameanguka kutoka kwa miti lakini wakifika hospitali, kwa sababu ni lazima wapelekwe hospitali za umma, ni lazima wafanyiwe ule upasuaji. Hawa wote ni watu ambao hali zao ni za chini. Baada ya mtu kufariki unapata anachukua karibu mwezi mzima pale kwa sababu familia haina uwezo wa kulipa ada ya hospitali."
}