GET /api/v0.1/hansard/entries/873907/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 873907,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873907/?format=api",
    "text_counter": 190,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kilifi South, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Ken Chonga",
    "speaker": {
        "id": 13374,
        "legal_name": "Richard Ken Chonga Kiti",
        "slug": "richard-ken-chonga-kiti"
    },
    "content": "Kwa hivyo, naunga mkono kikamilifu Hoja hii maanake wengi ambao wanategemea hospitali hizi hali zao ni za chini. Mhe. Ali amezaliwa na kulelewa Mombasa. Nimezaliwa kule chini vijijini ambako sikusikia umaskini lakini niliushuhudia. Ni wengi wanapata shida kwa sababu ya ada ambazo Serikali imezieka. Mbali na hayo, tunajua kwamba masuala ya afya yamepelekwa kwa kaunti. Kaunti zinashughulika kupata dawa na vifaa vya kukagua. Mbali na ada hizi kuondolewa, nasisitiza pia pesa ambazo zinapelekwa kwa kaunti kusaidia watu kwa minajili ya dawa, wauguzi na vifaa, ziongozewe ili kaunti ziweze kukimu mahitaji ya wale wengi ambao wanaathiriwa. Naunga mkono Hoja hii."
}