GET /api/v0.1/hansard/entries/873915/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 873915,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873915/?format=api",
"text_counter": 198,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kaloleni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Paul Katana",
"speaker": {
"id": 13357,
"legal_name": "Paul Kahindi Katana",
"slug": "paul-kahindi-katana-2"
},
"content": "Utafahamu kwamba punde tu mtu anapofariki katika hospitali za rufaa, mwili huzuiliwa kwa sababu ya malimbikizi ya ada za matibabu. Tunaomba pia Serikali ifutilie mbali ada zinazotozwa wakati mwili unahifadhiwa. Jamii nyingi haziwezi kulipa ada hizo za hospitali. Imekuwa ni vigumu sana kwa baadhi yetu Wabunge kwa sababu mwananchi anapopata tatizo kama hili, mtu wa kwanza anayemkimbilia ni Mbunge. Huwa hatuna pesa Serikali inatupatia ili tuweze kusaidia watu wetu. Kwa hivyo, naunga mkono Hoja hii ili Serikali ifutilie mbali ada za matibabu na ada ambazo zinatozwa wakati mtu amefariki. Pia, naongeza kuwa wakati mtu ametibiwa na ameshindwa kulipa ada, Serikali ifutilie ada hiyo ili asiendelee kukaa hospitali. Asante."
}