GET /api/v0.1/hansard/entries/873919/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 873919,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873919/?format=api",
"text_counter": 202,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nakuru Town East, JP",
"speaker_title": "Hon. David Gikaria",
"speaker": {
"id": 2489,
"legal_name": "David Gikaria",
"slug": "david-gikaria"
},
"content": ".Ametupatia takwimu na idadi ya madaktari waliopo na hii imetusaidia sana. Hoja hii ingepigwa msasa kidogo ndiyo iweze kusaidia wagonjwa wote ambao wako hospitali. Hoja inasema, “Bunge hili linahimiza Serikali ya kitaifa kufutilia mbali gharama zote za matibabu ya wagonjwa wote wanaofariki wakipokea matibabu katika hospitali za umma za rufaa.” Kama Hoja itapitishwa jinsi ilivyo, inamaanisha Wizara ya Afya itaweza kufuatilia hali vile ilivyo. Kuna mifano ya watu wengi. Ametoa mfano mzuri sana wa kijana mmoja ambaye mtoto wake wa mwezi moja alizuiliwa pale Kenyatta National Hospital (KNH). Kama vile Mohamed Ali amesema, mwanzo, alijaribu vile angeweza kuchangisha pesa kupitia marafiki lakini wakachanga Ksh2,000 pekee. Kwa hivyo, inaonyesha alikuwa na nia ya kutafuta hela aweze kutoa mtoto wake hospitalini. Ni mtoto wake wa kwanza. Mtoto wa kwanza ni mtoto wa maana sana. Sisemi wale wengine si wa maana. Mtoto wa kwanza huleta furaha katika familia. Huyu kijana alipojaribu kuchanga pesa, hakuweza kufikisha ada iliyotakikana. Alipofika pale, aliona njia mwafaka ni kutorosha mtoto. Mheshimiwa Ali anampongeza kwa wizi wa mtoto. Hatutauita wizi wa mtoto. Inasikitisha zaidi kwamba alifikishwa kortini. Yule jaji angeangalia hali yake. Katika hukumu, hawezi kupewa nafasi ya kujitetea. Kama hakungekuwa na msamaria mwema aliyekuja kulipa ada hiyo, hukumu ingekuwa namna gani? Bado hatia ni hatia. Tunapoangalia mambo haya pia tuongeze kwamba si wale wanaofariki peke yao - hili linahusu mtu yeyote ambaye anapata matibabu katika hospitali zetu za umma za rufaa. Wakati The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}