GET /api/v0.1/hansard/entries/873921/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 873921,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873921/?format=api",
    "text_counter": 204,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nakuru Town East, JP",
    "speaker_title": "Hon. David Gikaria",
    "speaker": {
        "id": 2489,
        "legal_name": "David Gikaria",
        "slug": "david-gikaria"
    },
    "content": "Tunapoongea kuhusu kubadilisha Katiba, hiki ni kitu cha kwanza ambacho tunatakikana kuangalie katika Fourth Schedule ambayo inaorodhesha majukumu ya serikali za kaunti na Serikali kuu. Ingawaje Mhe. Ali amepeana mfano wa Makueni, Gavana wa Makueni anaweza kufanya mambo haya yatendeke. Je, Gavana wa Makueni akiondoka, tupate mwingine ambaye atarudisha huduma za afya nyuma kule Makueni, itakuaje? Kwa hivyo, tusiangalie tu Makueni ama kule Machakos ambako tumesikia Gavana Mutua amelipa deni. Je, baada by muda wao kuisha, tutakuwa na magavana wagani? Pengine watakuwa kama waliopo sasa hivi. Kwa hivyo, ninataka kuunga mkono ndugu yangu Mhe. Ali kwamba huduma za afya ziwepo kutoka kiwango cha chini mpaka kule juu. Hospitali zetu za rufaa zinafaa zirejeshewe Serikali kuu. Ni muhimu kutaja kwamba sisi ndio tunapitisha Bajeti. Kama alivyosema ndugu yangu Mhe. Njomo, ni kweli sisi hupitisha Bajeti. Tumeanza huo mchakato wa kupitisha Bajeti. Ni jukumu letu kama Wabunge kuhakikisha pesa zimewekwa kwenye maeneo ya huduma ya afya. Serikali, kupitia Rais, imetoa mwelekeo juu ya vitu vinne ambavyo tunatakikana kuangazia. Jambo la kwanza ni afya. Kila mtu ataweza kupata huduma ya afya kama ilivyoelekezwa katika Katiba yetu. Kwa hivyo, sisi letu ni kuhimiza Wabunge wote, hasa Kamati ya Afya, kuangazia masuala ya Bajeti itakapoletwa ili tuelewe ni hela ngapi zinaekezwa katika huduma ya afya. Mwisho, na hii naomba wale ambao wanafanya mambo ya upelelezi, inatupatia hofu zaidi tunaposikia kuwa dawa ambazo zinatolewa kuhudumia wagonjwa katika hospitali za umma zinapatikana katika hospitali za kibinafsi. Hizo ni dawa ambazo zimegharamiwa na kulipiwa kwa bei ya juu lakini zinaibiwa na kupelekwa katika hospitali za watu binafsi. Ni jukumu la wapelelezi waweze kuangalia kwamba dawa zote ambazo zinatolewa kuenda hospitali zetu zinafika katika hizo hospitali. Ndugu yetu aliongea kuhusu kutoa damu. Hata kutoa damu siku hizi inakuwa shida. Hatuna damu ya kutoa katika miili yetu. Maisha yameenda chini. Ukimwambia mwananchi atoe"
}