GET /api/v0.1/hansard/entries/873923/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 873923,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873923/?format=api",
    "text_counter": 206,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nakuru Town East, JP",
    "speaker_title": "Hon. David Gikaria",
    "speaker": {
        "id": 2489,
        "legal_name": "David Gikaria",
        "slug": "david-gikaria"
    },
    "content": "moja ya damu, sijui kama ataweza kuishi wiki nyingine nzima. Zaidi ya hayo, hata si mambo ya kutoa damu. Nafikiri ni jinsi ambavyo tunaweza kuinua hali ya maisha ya Wakenya. Siku hizi tunaenda kutoa damu kunapotokea janga lakini zamani ninakumbuka tukiwa shuleni, tulikuwa tunatoa damu wakati wote. Mtu alikuwa anaenda kwa hiari yake kutoa damu. Lakini siku hizi tunangoja mpaka janga lipatikane ndio tutoe damu. Kila mtu anahofia namna damu inavyotolewa. Sisi Wabunge tulialikwa siku moja hapa Uhuru Park tutoe damu na wengi wetu hatukuenda. Mimi nilienda pale lakini sikufikiwa. Kulitokea mambo mengine. Kwa hivyo, ni muhimu nimshukuru Mheshiiwa Ali kwa kuileta Hoja hii. Tukishapitisha mambo haya, tunaomba Kamati ya Utekelezaji ambayo inaongozwa na ndugu yetu, Mheshimiwa ole Kenta, wafuatilie mambo ambayo tumekubaliana katika Bunge. Kama tumekubaliana hizi ada ziondolewe, Kamati ya Utekelezaji lazima ifuatilie kwa hospitali 11 ambazo Mhe. Ali alitaja ili ziweze kufuata maagizo ya Bunge na kuondoa gharama ambayo ndugu yetu alikuwa akiongea kuhusu. Kwa hivyo tutaomba Kamati ya Utekelezaji, kama Hoja hii itapitishwe, ifuatilie mambo haya mara moja ndiyo isiwe tunaongea tu. Asante. Ninaunga mkono Hoja hii."
}