GET /api/v0.1/hansard/entries/873926/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 873926,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873926/?format=api",
    "text_counter": 209,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ganze, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Teddy Mwambire",
    "speaker": {
        "id": 13334,
        "legal_name": "Teddy Ngumbao Mwambire",
        "slug": "teddy-ngumbao-mwambire-2"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi ya kuchangia Hoja hii ambayo iko mbele ya Bunge hili. Ninaunga mkono Hoja ambayo imeletwa na ndugu yetu, Mbunge wa Nyali. Hii ni Hoja ambayo ina mshikamano zaidi hususan kwa wale watu ambao wanaishi kwa umaskini ambao tunawaakilisha. Mbunge wa Nyali ameongea kuhusu hospitali za ngazi ya tano, lakini swala hili linastahili liweze kuenda chini kama vile hoipitali za ngazi ya nne. Ngazi hizo ndizo huwa na watu wengi ambao wanaaga dunia na miili yao inazuiliwa. Pia Hoja hii imependekeza kuwa ada ya matibabu itolewe. Ni muhimu pia kusiwe na ada ya kuhifadhi miili. Kule ninakotoka, kuna wale ambao wanauwawa, kuna wale ambao wanakufa na kuna wale ambao wanapata ajali. Wale wote wanauwawa kwa ajali, ni lazima wapelekwe katika hifadhi za maiti ili waweze kufanyiwa uchunguzi vizuri. Sasa kama wamepelekwa kwa hifadhi za maiti na ilikua ni ajali ya ghafla ambayo mtu ana uwezo wa kukinga au kujipanga, inakuwa vigumu sana kutoa mwili ili kuuzika baada ya ule muda wa kufanya utafiti umepita. Mhe Spika Naibu wa Muda, ningependekeza kuwa Mhe. Ali aweze kufikiria mbali na matibabu, kuwe na pesa za kuhifadhi miili ili kuhifadhi miili kusichukue muda mrefu kama ilivyo sasa hivi. Kuna matatizo makubwa sana kwa wale wataalam ambao hufanya utafiti kwa miili maana hospitali nyingi za ngazi ya nne hufanya utafiti siku moja kwa juma, kwingine utasikia ni siku ya alhamisi peke yake, na kwingine utasikia ni jumatano peke yake. Nafikiri tumepata shida nyingi sana kabla ya Katiba tuliyo nayo sasa kuletwa. Nimesikia wenzangu wakiongea kuhusu serikali gatuzi na mamlaka zilizo nazo hususan kwa maswala ya matibabu kwamba hawawezi kutimiza wajibu wao. Kwa hivyo, huduma ile iweze kutolewa na ipelekwe kwa Serikali kuu. Ukitembea katika kaunti nyingi, utapata kwamba serikali nyingi za gatuzi zimejaribu kujikimu katika kupeana huduma ya afya. Matatizo ambayo yalikuweko ambayo tunatakikana kuyaangalia kwa kina ni kwamba Serikali haikua imekumbatia ugatuzi kwa ukamilifu na ndio maana kulikuweko na mambo ambayo yalifanyika kwa Serikali kuu ambayo yaliathiri huduma katika serikali gatuzi. Kwa mfano, vifaa vya kuchunguza wagonjwa tofauti vilinunuliwa na wizara. Serikali gatuzi nyingi zinalipa madeni makubwa kwa sababu ya mpango uliopangwa na Serikali kuu. Kwa hivyo, Serikali kuu inafaa kusaidia serikali gatuzi ili ziweze kutoa huduma bora zaidi kama vile ambavyo wamekuwa wakidai kupitia serikali gatuzi kuhusu swala la akina mama kujifungua ili tuweze kupata huduma ambazo zinastahili kupatikana. Tukisema ya kwamba ada itolewe, ningesema kwamba kuna umuhimu wa kuongeza zahanati, ili serikali gatuzi iweze kuzihudumia kikamilifu. Kuna wenzangu ambao wamesema Wabunge wa kitaifa hawawezi kuhusika na kujenga zahanati. Kuna zile pesa za usawawishaji. Waingereza wanaiita Equalisation Fund . Najua kwamba pesa hizi zinatumika kwa kujenga zahanati. Kule Ganze, tunajenga zahanati kadhaa. Baada ya kujenga zahanati au hosipitali, itabidi majengo yale yapewe serikali gatuzi ili waweze kuziendeleza, kuajiri, kuleta dawa na kutoa huduma kamilifu. Hayo ndiyo maswala ambayo yanaweza kufanyika. Kwa hivyo, tuweze kuangalia peo tofauti. Tunaweza kutumia majukumu yetu kuona jinsi tutaweza kuboresha afya. Kama Serikali ina nia ya kuboresha maswala ya afya, itaboreshwa na tutahakikisha kwamba tunapata huduma bora. Ni hakika kwamba baada ya kupitisha Hoja hii, wale wenzetu ambao wako katika bunge za kaunti na wale ambao wako katika Seneti, tuhakikishe kwamba huduma hii inaelewa kikamilifu. Musukumo wa Serikali kuu pekee hauwezi kufaulu. Kule chini kuna watu ambao wanastahili kuwa waangalifu wa karibu, ili tuone kwamba hii huduma inapatikana. Sasa hivi, The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}