GET /api/v0.1/hansard/entries/873931/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 873931,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873931/?format=api",
    "text_counter": 214,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kajiado North, JP",
    "speaker_title": "Hon. Joseph Manje",
    "speaker": {
        "id": 1669,
        "legal_name": "Joseph Wathigo Manje",
        "slug": "joseph-wathigo-manje"
    },
    "content": "Nilikuwa nikisema kulikuwa na kijana mmoja ambaye aliambia mke wake aende hospitali KNH. Baadaye, alishindwa kulipa Kshs56,000 ambayo ilikua ada ya hospitali. Kijana huyu, ambaye anatoka Eneo Bunge langu la Kajiado Kaskazini, aliona ni heri aweke mtoto wake kwenye mfuko ili watoroke hospitalini. Alishikwa na kupelekwa mahakamani lakini wasamaria wema walichangia na akawa huru. Hii ni kusema ya kwamba alifikiria hivi kwa sababu hakuweza kulipa ada hiyo. Hili ni jambo ambalo hutendeka kila wakati. Wabunge wote watakuambia kuwa wakienda mashinani, huwa wanapata shida hizi. Kesho nikienda ofisini kwangu, sitakosa mtu ambaye ataniambia ya kwamba kuna maiti hospitalini ambayo imezuiliwa kwa sababu hawawezi kulipa ada ya hospitali. Mtu akifariki amefarika. Familia yake imepoteza. Wakifuatiliwa zaidi, wanaendelea kupoteza zaidi. Ni muhimu tujaribu vile tunaweza kuchangia hata ikiwa ni wakati wa Bajeti tuone vile hosipitali zinapatiwa kiwango fulani cha kuhudumia mtu akifariki. Wakati mtu amefiwa na anaendelea kuwekewa maiti hospitalini ni kama kwamba kifo hicho kinaendelea. Matatizo yale yanaendelea. Ni kama kupoteza mara mbili. Wakati mwingine, inaonekana kama Serikali imechangia kwa sababu anapelekwa hospitalini na wakati mwingine hakuna dawa. Wakati mwinigine kuna migomo ya wauguzi na wagonjwa hawahudumiwi vizuri na hiyo inasababisha kifo. Wagonjwa wakifariki, Serikali inafaa kungana na familia zao. Pia, kuna magonjwa mengine kama saratani ama ajali za barabara ambazo hupatikana wakati watu hawatarajii. kwa hivyo, ni muhimu tuangalie chanzo cha vifo hivi. Kuna mjadala unaosema kuwa wananchi wawe na kadi ya NHIF. Si watu wengi wana uwezo wa kugharamia kadi hizi. Mia tano kwa mwezi ni pesa nyingi kwa wakenya maskini na ingekua ni vizuri tujaribu juu chini tuhakikishe kwamba tumepunguza ada ya hospitali. Siyo tu miili ambayo inazuiliwa hospitalini, mtu akitibiwa na hana uwezo wa kulipa ada, hakuna haja aendelee kuzuiliwa hospitalini na familia yake haiwezi kulipa hiyo gharama. Mtu akifariki, familia inauza shamba ama wanaitisha harambee ili kulipa ada ya hospitali. Katika eneo Bunge langu kuna kijiji kinaitwa Majengo ambako mama mmoja alipoteza mtoto wake. Huyu mama akawa na deni ya Kshs500,000. Familia ikafikiria kufanya mchango na wakapata Kshs20,000. Ikawa hawajafanya kitu. Ilibidi waje kwangu. Tukamwandikia social worker ili tuangalie kama The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}