GET /api/v0.1/hansard/entries/873932/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 873932,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873932/?format=api",
"text_counter": 215,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kajiado North, JP",
"speaker_title": "Hon. Joseph Manje",
"speaker": {
"id": 1669,
"legal_name": "Joseph Wathigo Manje",
"slug": "joseph-wathigo-manje"
},
"content": "hiyo maiti ingeweza kuondolewa KNH. Tulifanya hivyo kwa sababu waliandaa harambee nne na hawakuweza kupata pesa za kulipa ile ada ili wapate ule mwili. Nikimalizia, ni vizuri tuangalie ile ahadi tuliwapa Wakenya ya kwamba kutakuwa na matibabu ya bure, haswa kwa ngazi ya pili na tatu. Lakini unakuta matibabu ni duni na inabidi wagonjwa wahamishwe katika hospitali zingine. Wanafariki kwa sababu wamezidiwa sana. Wale ambao wanahamishiwa wana mapato ya chini na wakifariki familia zao zinashindwa kuchukua miili yao ili kuizika. Ninaunga mkono Hoja hii. Huu ni mjadala mzuri sana. Hoja hii ikipita, Waheshimiwa wengi wakirudi ofisini zao na kuona watu wamepanga laini, haitakuwa ni kwa sababu ya mambo ya maiti zilizozuiliwa hospitalini. Pia, katika hospitali za umma kama Mama Lucy Hospital, gharama iko juu sana na inafika haka kiwango cha Kshs2 milioni. Familia zinashindwa kulipa ada hizo na hawana njia nyingine. Hospitali zinazuilia miili ya wafu na familia zinawasumbua Waheshimiwa na hatuna pesa za jambo hilo. Asante. Ninaunga mkono."
}