GET /api/v0.1/hansard/entries/873968/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 873968,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873968/?format=api",
"text_counter": 251,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kilifi CWR, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Gertrude Mwanyanje",
"speaker": {
"id": 13245,
"legal_name": "Gertrude Mbeyu Mwanyanje",
"slug": "gertrude-mbeyu-mwanyanje"
},
"content": "Imefika wakati tuweze kutetea jamii zetu waweze kuachiliwa kutolipa ada hizi za magonjwa kama haya na mengineo. Hali ya uchumi hapa Kenya imekuwa juu sana. Watu hawawezi hata kumudu chakula cha kila siku. Mtu asile asubuhi, mchana na usiku pia kupata chakula ni shida. Ukimwambia alipe matibabu ya Kshs250,000 kwa hospitali kwa sababu ni mgonjwa wa pressure ama sukari, inakuwa ni hali ngumu. Kwa hivyo, nataka kumpongeza Mhe. Mohamed Ali kwa kuileta Hoja hii. Matibabu yamegatuliwa na hospitali nyingi zetu za umma katika gatuzi zetu zimefikia kiwango ambacho haziwezi kuwekeza huduma za afya. Wakati umefika katika Bunge hili tufanye kazi pamoja ili huduma zinazofaa zifikie watu wetu. Nitakupatia mfano mmoja. Kuna mwalimu mmoja kutoka Eneo Bunge la Ganze anayeitwa Mr. Kahindi. Alifariki miezi miwili iliyopita na mwili wake uko katika mochari moja kule Mombasa kwa sababu ana deni la Kshs3 milioni. Tumechanga lakini imeshindikana na familia haiwezi kabisa. Ninaomba kupitia Hoja hii kuwa familia hii isaidiwe na Serikali ili waweze kuuzika ule mwili. Deni lile la Kshs3 milioni ni kubwa sana kwa ile familia ambayo haiwezi kujimudu chakula. Itakuwa ni gharama ya kila siku. Hawataweza kuuzika mwili wa mwalimu yule. Kwa hivyo ninaomba, kupitia kwa Hoja hii, Serikali iweze kusikia kuhusu mwalimu huyu, Mr. Kahindi, kutoka kule Kachororoni, Ganze, ndio familia yake ipatiwe mwili wake ili waweze kuuzika na wapumzike huzuni ya miezi miwili. Mpaka sasa, hawajaweza kuuzika ule mwili. Niko na mengi lakini kama hizi ada za hospitali na mochari zitaweza kuondolewa, sisi na wananchi wetu tutaweza kufanya mambo mengine ya kimaendeleo. Pesa nyingi zinatumika katika kuzingatia mambo ya mazishi ya wale kaka, ndugu na mama zetu wanaofariki na kuhifadhiwa kwa muda mrefu kwa sababu ya ada za hospitali. Asante sana, Mhe. Naibu Spika."
}