GET /api/v0.1/hansard/entries/873970/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 873970,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873970/?format=api",
    "text_counter": 253,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nyandarua CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Faith Gitau",
    "speaker": {
        "id": 974,
        "legal_name": "Faith Wairimu Gitau",
        "slug": "faith-wairimu-gitau"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ninataka kumshukuru kakangu, Mhe. Mohamed Ali, kwa kuileta Hoja hii ya kufutilia mbali ada za matatibu katika hospitali za umma na za rufaa pindi mtu anapofariki. Kama Jimbo la Nyandarua, tuko na hii shida kila wakati. Watu wanakufa katika hospitali ya KNH na watu wao hawawezi kulipa ada ya hospitali. Juzi kulikuwa na mama mmoja ambaye ada yake ilikuwa Kshs5 milioni. Familia yake haingeweza kulipa ada hii na alikaa kwa chumba cha kuhifadhia maiti kwa mwaka mmoja tukitafuta pesa za kulipa hiyo ada ya hospitali. Kwa hivyo, hii ni shida kubwa sana. Pia, inaonekana kwamba majimbo yetu hayana namna ya kuendeleza hospitali. Ukiangalia hospitali zetu nyingi hazina dawa, nesi na madaktari. Kwa hivyo, ninaomba ikiwa kaunti zetu zimeshindwa na kazi hii ya kuendeleza masuala ya afya, zirudishe kwa Serikali Kuu kwa sababu Serikali inaweza kuhakikisha kwamba maneno yote yameangaliwa vilivyo. Mimi naunga mkono Hoja hii na kusema kwamba kuna ajali ambazo zinafanyika katika barabara zetu. Kukifanyika ajali barabarani, watu wanachukuliwa na kupelekwa hospitali ile iko karibu. Mara nyingi hospitali hizi ni za kibinafsi. Wanawekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kwa siku mbili au tatu. Mtu huyu akifariki watu wao hawana pesa za kumtoa katika hospitali hiyo ya kibinafsi. Kwa hivyo, ni shida kubwa sana. Tunaomba sisi Wabunge tushikane tulete Mswada kwa sababu mara nyingi naona Hoja nyingi zinazoletwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}