GET /api/v0.1/hansard/entries/873975/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 873975,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873975/?format=api",
    "text_counter": 258,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nyandarua CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Faith Gitau",
    "speaker": {
        "id": 974,
        "legal_name": "Faith Wairimu Gitau",
        "slug": "faith-wairimu-gitau"
    },
    "content": " Asante sana. Najua rafiki yangu anapenda sana kutetateta. Ameteta kutoka asubuhi mpaka saa hii hajanyamaza. Kwa hivyo tutaendelea tu. Tumemzoea lakini hata mimi utanizoea na hiki Kiswahili changu cha kule Nyandarua. Najua naongea vilivyo. Hata rafiki yangu, Mhe. Mohamed Ali, ananiyoshea kidole kwa sababu naongea lugha sanifu kabisa. Naomba kuunga mkono Hoja hii. Lazima hospitali zetu ziache maneno haya ya kufungia miili mwaka mmoja au miezi kadhaa kwa sababu ada hazijalipwa. Kama Mheshimiwa alivyosema, madaktari wetu watakuwa wakiwatibu watu haraka kwa sababu wasipowatibu na mtu afe katika hospitali yake, hatalipwa pesa yake kama daktari. Naunga mkono pendekezo hilo kwa sababu sasa madaktari watakuwa wanatia makini kutibu watu kwa sababu watu wengi wanakuwa misdiagnosed . Hiyo sijui ni nini kwa Kiswahili. Wanakuwa misdiagnosed na wanatibiwa magonjwa hawako nayo kama kifua kikuu au saratani. Hata saratani ingeitwa shetani kwa sababu huo ndio ugonjwa ambao unamaliza watu nchini. Kama kwetu Nyandarua, kila siku unasikia kuna mtu anaugua ugonjwa wa saratani. Watoto wengi wako hospitali ya Kenyatta. Sio eti unashika tu wazee. Siku hizi unashika hata watoto wa miezi miwili au tisa. Juzi tulizika mmoja wa miaka tisa ambaye ugonjwa huu ulimshika mdomoni. Lazima maneno yote yaangaliwe. Watu wengi wamezuiliwa katika vyumba vya kuhifadhi maiti. Serikali lazima kutoka kesho iwaachilie. Asante sana. Naunga mkono Hoja hii."
}