GET /api/v0.1/hansard/entries/873977/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 873977,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873977/?format=api",
    "text_counter": 260,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mwatate, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Andrew Mwadime",
    "speaker": {
        "id": 2451,
        "legal_name": "Andrew Mwadime",
        "slug": "andrew-mwadime"
    },
    "content": " Shukrani, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Mwanzo kabisa, naunga mkono Hoja hii. Sura ya nchi ni lishe bora, mazingira bora na matibabu bora. Vilevile, kabla sijasahau, ni vyema Bunge hili lifikirie sana sheria za nidhamu kwa sababu kuchanganya lugha ya Kiswahili na Kiingereza iko kila mahali. Ndio maana Bunge la Tanzania limechangamka kuliko hili letu kwa sababu Wabunge wengi hawawezi kuongea Kiingereza moja kwa moja na pia hawawezi kuongea Kiswahili moja kwa moja. Hiyo ni changamoto. Kando na changamoto za lishe bora na mazingira bora, matibabu nchini yamekuwa kizaazaa kikubwa mno. Sasa hivi, Wabunge wengi wanatumia mishahara yao kulipia madawa hospitalini ama kuchangia mazishi. Limekuwa suala nyeti sana hapa nchini. Utapata Jumamosi moja mnazika watu zaidi ya kumi hata mtu anakuwa na wasiwasi ilhali sote ni mali ya Serikali. Kuna Muingereza mmoja ambaye alikuwa anaitwa Maslow aliyeandika kuhusu mahitaji ya binadamu. Aliorodhesha mahitaji madogo madogo hadi mahitaji makubwa makubwa. Matibabu ni katika mahitaji madogo madogo kama vile lishe lakini hapa nchini ninashangaa kwa sababu kodi tunazotoa kwa mwaka zinafikia zaidi ya Sh1,000 bilioni tena zaidi ya mara tatu. Ni The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}