GET /api/v0.1/hansard/entries/873978/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 873978,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873978/?format=api",
    "text_counter": 261,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mwatate, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Andrew Mwadime",
    "speaker": {
        "id": 2451,
        "legal_name": "Andrew Mwadime",
        "slug": "andrew-mwadime"
    },
    "content": "kwa sababu hakuna mpangilio sawasawa. Kungekuwa na mpangilio sawasawa na ufujaji usiwepo, Serikali ingekuwa inaweza kutibu watu wake bila hata kuomba hela za madawa au za matibabu na hata kama unahifadhi mwili mtu anapofariki. Sisi tumelegea katika upande huo. Hela inayohitajika kutibu Wakenya wote haiwezi kuzidi Sh500 bilioni. Haya ni mahitaji ya kila mwananchi. Sasa hivi ukiangalia hospitali zote nchini, sio za rufaa tu bali hata zile za umma kule mashinani, taabu ni hizo hizo. Kwangu nyumbani niko karibu na zahanati nyingine hapo. Ni kizaazaa. Hamna hata kutulia. Hili ni suala ambalo watu wanafaa kulichukulia kwa undani na walifikirie sawasawa. Nampa Mbunge wa Nyali pongezi kwa kuleta Hoja hii. Ubaya wetu tunatoa Hoja tamu tamu kama hizi lakini kesho kutwa utakuta imepotea. Hakuna mtu ataongezea. Kamati tekelezi haifuatilii. Inakuwa tu tabia ya kuongea masuala mazuri kama haya. Nchi nyingine wanaiga na wanatelekeleza na sisi bado tuko pale pale. Wakenya wanaumia. Ukiwauliza Wabunge wengi hapa hata sasa hivi kuna mmoja hapa alikuwa ananiitisha hela aende tu hapa kwa sababu hana chochote. Najua ni kwa sababu ya masuala kama haya. Kamati ya Bajeti iketi chini na ifikirie suala hili kwa kina na sio kuongea tu na kupata bonga points katika Bunge hili na katika runinga halafu tunaachilia suala hili hivi. Nampongeza sana Mbunge wa Nyali maana ni mbunifu. Ameleta Hoja ambayo inaweza kuwasaidia Wakenya, hasa wale ambao hawajiwezi. Singependa kuongea mengi. Shukrani kwa kunipa fursa hii. Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}