GET /api/v0.1/hansard/entries/873980/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 873980,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873980/?format=api",
"text_counter": 263,
"type": "speech",
"speaker_name": "Trans Nzoia CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Janet Nangabo",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": " Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi ya kuchangia Hoja hii iliyoletwa na Mbunge mwenzetu, Ali Mohamed. Namshukuru sana kwa Hoja hii. Imekuja wakati mzuri kwa sababu maeneo ambayo baadhi yetu tunatoka, watu wanaumia sana. Mwenzangu Oluoch alichangia na kusema kwamba kulikuwa na hospitali moja katika eneo langu kule Trans Nzoia, Crystal Hospital iliyomtoza ada mtu ambaye alikuwa ameumia katika sehemu hizo Ksh200,000. Kijana huyo anayeitwa Wanjala, alikuwa anaishi maisha ya umasikini na upweke. Hakika, hangeweza kulipa hiyo ada na ndiposa inatulazimu sisi kama viongozi kutafuta marafiki wenzetu na tuungane pamoja kuhakikisha kwamba tunamchangia pesa za kumsaidia. Sio yeye peke yake katika hospitali hiyo, walikuwa wengi mno. Kuna mama kutoka sehemu yangu aliyekuwa anaugua ugonjwa wa saratani na familia yake ikatozwa Ksh674,000 lakini alipoteza maisha yake. Sisi kama viongozi ama wenyeji katika sehemu hizo hatuwezi kujimudu kutoa hizo pesa kumsaidia mama huyo. Ndiposa namshukuru Mhe. Ali kwa kuleta Hoja hii ili tuichangie. Tuna uhakika kwamba wale wanaohusika na mambo ya afya katika nchi yetu wanatusikiza. Mwaka uliopita, nilileta Hoja kuhusu akina mama wenzetu ambao baada ya kupata mimba ya mapema ama kujifungua, huwa wanaathirika na ugonjwa unaoitwa fistula. Nashukuru sana kwa sababu Mama Margaret alishikilia mara moja na saa hii, watu wanapata matibabu katika nchi yetu. Vile vile, tunapoijadili Hoja hii katika Bunge hili, nina imani kwamba Waziri anayehusika na mambo ya afya atahakikisha kwamba amesaidia Wakenya wasiojiweza kwa kulipa ada hiyo wakifariki. Hata kama wengine hawajafariki lakini hawajimudu kimaisha, ahakikishe kwamba ada hiyo imeondolewa mbali. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}