GET /api/v0.1/hansard/entries/873981/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 873981,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873981/?format=api",
"text_counter": 264,
"type": "speech",
"speaker_name": "Trans Nzoia CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Janet Nangabo",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": "Hivi juzi kulikuwa na janga la magaidi pale Riverside. Kuna watu ambao hawangeweza kujimudu hata kulipa ada katika hospitali na ikamulazimu Seneta wa Kaunti ya Nairobi kutoa pesa zake katika mfuko wake kumlipia yule aliyekuwa ameathirika. Kuna wengi ambao hawawezi kutufikia sisi viongozi. Vile ambavyo wengine wamechangia hapa, kuna walemavu miongoni mwao. Kuna wale wametoka katika maisha ya upweke na hawawezi kutufikia sisi viongozi kuwasaidia na senti kidogo kuhakikisha kwamba wanapata matibabu kama watu wengine. Nawaunga wenzangu mkono kwa sababu wakati tunapewa nafasi hii kama viongozi katika Bunge hili, haimanishi kwamba sisi ni matajiri. Sisi pia tumetoka katika maisha ya upweke. Wengine tumepoteza wapendwa na hatuwezi kujimudu kama viongozi. Tunawapatia watu mwelekeo katika maisha yao na wale wananchi ambao wametupa kura kama viongozi wao. Kuna wenzetu ambao wamekuwa katika Bunge hili ambao kule nje, wanapata taabu sana. Upande wa magharibi ya Kenya, huwa wanategemea kilimo cha miwa. Lakini wakati huu, wakulima kutoka eneo hilo hawana lao la kusema kwamba wanajivunia. Hawana senti za kupeleka wagonjwa wao hospitalini. Katika Bonde la Ufa, wengi wanategema mahindi yao. Wakiwa na wagonjwa ama wapoteze wapendwa wao na watoto wao katika eneo hilo, tegemeo lao lilikuwa ni mahindi. Tutoe senti wapi kwa sababu watu hawajimudu? Ndiposa namuunga mkono mwenzangu, Ali. Nawashukuru watu wa Nyali kwa kukupa nafasi hii kuja katika Bunge hili kuleta Hoja kama hii. Tunatarajia kwamba Kamati ya Bunge hili ya Utekelezaji itahakikisha kwamba imetenda vilivyo. Sisi tutafurahi. Tunawahimiza wale wanaoshikilia Bajeti katika Bunge letu, wakipata kama mambo ya afya… Yule gavana katika kaunti yangu hajawahi kuja katika Bunge hili. Huenda ikawa alipewa nafasi katika kaunti hiyo kwa sababu ya mrengo ama bahati yake. Licha ya kupata fedha nyingi, watu hawa huwa hawaangalii masilahi ya wale masikini walio huko chini. Ni sisi katika Bunge hili tunaofanya hivyo kwa sababu tunapoongea, watu wanasikiza. Tutekeleze mambo mengine katika Serikali ya kitaifa na tuhakikishe tunapopeleka ujumbe kule mashinani, tunaongea na watu walio na afya nzuri. Katika eneo langu la Trans Nzoia kuna squatters wengi sana. Hawana lao. Ukisema mtu aende hospitalini, hana chochote. Asubuhi akiamka aje kwangu, hatafika kwa sababu hana pesa ya kupanda ile pikipiki ama kutumia baiskeli mpaka kwangu. Iwapo ni mgonjwa, mtu huyu atasaidika namna gani? Vyumba vya kuhifadhia maiti vimejaa kwa sababu ya mgomo wa madaktari katika nchi yetu. Kama viongozi tunataka tushikilie msimamo wa kuhakikisha kwamba masuala ya madaktari yameshughulikiwa. Ninamsihi Rais. Licha ya kusema kwamba ametoa amri, awe na mikakati mwafaka ya kuhakikisha kwamba ile amri anatoa anielekeza panapotarajiwa. Tunapoteza wapendwa hapa nchini. Kila Jumamosi, watu hututumia ujumbe kwamba wamepoteza wapendwa wao. Tutoe wapi fedha? Sisi hatuna pesa za kutosha. Nawaomba wenzangu waunge mkono Hoja hii. Mwenzetu Ali alete Mswada katika Bunge hili ili tutenge pesa za kuhakikisha kwamba tunawasaidia wale ambao wamekuwa na shida kama hii. Kuna wale wameumia kama yule kijana Boniface. Nawashukuru wasamaria wema waliojitolea kuhakikisha maisha ya kijana huyo yataendelea mbele. Naunga mkono Hoja hii."
}