GET /api/v0.1/hansard/entries/873995/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 873995,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873995/?format=api",
"text_counter": 278,
"type": "speech",
"speaker_name": "Tetu, JP",
"speaker_title": "Hon. James Gichuhi",
"speaker": {
"id": 13490,
"legal_name": "James Gichuhi Mwangi",
"slug": "james-gichuhi-mwangi"
},
"content": " Mhe. Naibu Spika wa Muda, nilisikiza vizuri Mhe. Mohamed Ali alipokuwa akichangia. Kwanza kabisa, alitambua Ibara ya 43 ya Katiba ambayo inasisitiza umuhimu wa kupata matibabu ya bure. Ibara ya 43 ya Katiba inazingatia umuhimu wa kupata matibabu ya bure. Hiyo ni haki. Ningesisitiza kwa Kamati ya Afya, kuwe na sheria ambazo zinazingatia umuhimu wa kupata matibabu ya bure katika hospitali za umma zote. Nilisoma juzi ya kwamba kaunti ya Lamu iliita madaktari kutoka Uspania ambao walikuwa wanapeana matibabu ya bure. Kwa wiki tatu, kulikuwa na watu kama 400 ambao walijitokeza ili wapate matibabu ya bure. Hiyo ni ishara ya kwamba kama tungekuwa na sheria ama kama tungekuwa tunatibiwa katika hospitali za umma bila kulipa pesa zozote, tungekuwa tunazuia vifo. Mtu anapata maumivu kwa mwili na anaogopa kwenda hospitali kwa sababu hana pesa. Anaenda kwa duka, ananunua dawa na anajitibu. Kama hakuna pesa ambazo mtu analipa akienda hospitali wakati tu amepata maumivu, anaenda hospitali na anapata matibabu, angezuia kifo. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}