GET /api/v0.1/hansard/entries/873996/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 873996,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873996/?format=api",
"text_counter": 279,
"type": "speech",
"speaker_name": "Tetu, JP",
"speaker_title": "Hon. James Gichuhi",
"speaker": {
"id": 13490,
"legal_name": "James Gichuhi Mwangi",
"slug": "james-gichuhi-mwangi"
},
"content": "Tunaona wakati mwingi watu wanaenda hospitali wakati wamepata maumivu kabisa ndio wanafanya mchango. Juzi nilikua na kesi ya mgonjwa fulani kutoka eneo langu la Tetu. Aligonjeka akapelekwa Hospitali ya Kenyatta halafu akaaga dunia. Alikua na ada ya Kshs800,000. Nilichanga pesa kidogo lakini maiti ilikaa kwa chumba cha kuhifadhi maiti kwa zaidi ya mwezi mmoja. Juzi tu ndio tulipata pesa na tukaweza kuzika maiti."
}