GET /api/v0.1/hansard/entries/873997/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 873997,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/873997/?format=api",
    "text_counter": 280,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Tetu, JP",
    "speaker_title": "Hon. James Gichuhi",
    "speaker": {
        "id": 13490,
        "legal_name": "James Gichuhi Mwangi",
        "slug": "james-gichuhi-mwangi"
    },
    "content": "Uingereza ni mfano mwema wa nchi ambayo imeendelea. Wananchi wa Uingereza wanapata matibabu ya bure na kila mtu ako na dakitari wake. Najua sisi kama Wabunge tunaweza kuunda sheria. Tunaweza kuwa na sheria zitakaoifanya iwe ni lazima kila mtu apate matibabu ya bure. Tukipata matibabu ya bure idadi ya watu wanaoaga dunia itakuwa ya chini. Pia,mtu akipata matibabu ya bure na kwa bahati mbaya aage dunia, inastahili asilipe pesa yoyote hata ada ya chumba cha kuhifadhi maiti. Tukifanya hivyo, kama Wabunge, tutakuwa tunaiunga Serikali mkono. Tutakua tumesaidia wananchi ambao wametuchagua. Jambo muhimu ni kuwa na afya njema. Ndiposa imeekwa kwa Katibu kama haki ya binadamu."
}