GET /api/v0.1/hansard/entries/874006/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 874006,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/874006/?format=api",
"text_counter": 289,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kajiado CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Janet Teyiaa",
"speaker": {
"id": 13239,
"legal_name": "Janet Marania Teyiaa",
"slug": "janet-marania-teyiaa"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nichangie Hoja hii ambayo imeletwa na Mhe. Mohamed Ali kuhusiana na kuondolewa kwa ada mtu anapofariki. Tunajua matibabu ni jambo la maana sana kwa jamii lakini tumekuwa na shida kubwa kwa hali ya matibabu. Mara nyingi watu wanakufia hospitali ambapo wanaacha deni kubwa sana. Familia nyingi ni maskini, hawawezi kupata hii pesa. Tunaishi kwa harambee kila siku na mara nyingi hata hiyo haipatikani na watu wanaumia. Mali inaenda na bado wanakatazwa kuzika wapendwa wao. Hii pesa ikiondolewa, itatusaidia sana kila mahali. Watu wengi huona Kaunti yangu ya Kajiado kama ni tajiri lakini kuna umaskini sana. Tuko na vijiji na wanoishi humo ni maskini sana. Hata chakula mtu hapati wacha kuenda hospitali. Tunajaribu kuwahamiza wapate hii kadi ya hospitali lakini hata hiyo pesa ya kuweka hawapati. Mara nyingi wanaumia sana. Hatusemi watu wasilipe pesa kabisa, lakini kuwe na kiwango ambacho mtu wa kiwango cha chini anaweza kufikia. Tunajua watu wana uwezo tofauti. Kuna watu ambao wako na kazi, wengine hawana, wengine ni maskini kabisa na wengine wako katikati. Ni vizuri wote waweze kupata matibabu inayofaa. Tunapoongea kuhusu matibabu, ni muhimu kuzingatia zile zahanati za mashinani. Mara nyingi, haziwezi hata kutoa huduma za dharura. Watu wanaumia, wengine wanaishi mashinani na hawawezi kupata hospitali za rufaa na wanafariki. Ni vizuri Serikali iweze kutenga pesa ama vifaa vinavyofaa kutoa huduma za dharura ili watu wakiwa na shida wapate kuhudumiwa kwa njia inayofaa. Kabla wafike katika hospitali za rufaa, wengine hufia njiani. Wengine wanaishi mbali sana na hospitali hizi na wakati mwingine, hawana gari ya kuwasaidia wafike huko. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}