GET /api/v0.1/hansard/entries/874009/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 874009,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/874009/?format=api",
    "text_counter": 292,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kinango, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Benjamin Tayari",
    "speaker": {
        "id": 13379,
        "legal_name": "Benjamin Dalu Stephen Tayari",
        "slug": "benjamin-dalu-stephen-tayari-2"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili niweze kuchangia Hoja hii inayohusu mambo ya kutolipisha wananchi ada mtu anapofariki. Katika sehemu ambazo tunakotoka, tunajua kwamba watu wengi ni maskini sana katika jamii zetu. Ule umasikini unaongezewa zaidi na gharama ya kulipa matibabu ya magonjwa tofauti tofauti. Tunaona matibabu ambayo wengi wanafuatilia katika hospitali za rufaa ni kama magonjwa ya saratani, sukari na pressure na mengine kama vile kuvunjika miguu kwa ajali za pikipiki. Wengi wanapooaga dunia, tayari huwa wametumia pesa nyingi sana kulipia huduma zile wanazopatiwa katika hospitali zile. Wakiongezewa mzigo wa kuhakikisha kwamba ni lazima pesa yote wanayodaiwa kuwa tayari, umewatia katika hukumu. Hivi juzi tuliona aibu kama Serikali baada ya kuona kuwa jamii wanakimbia na watoto kwa sababu ya ada ambazo zimewekwa hospitalini. Ningeomba Bunge hili lisisitize umuhimu wa kuona ya kwamba tunalinda jamii yetu, hususan wale ambao wanatafuta matibabu katika hospitali za rufaa wakiwa katika hali ambayo hawajiwezi. Hospitali kama vile Makadara ama Coast General kule Mombasa, utapata kuwa wagonjwa wametolewa kwa vitanda na kulazwa chini, kwa sababu hawawezi kulipa. Wengi hutafuta Wabunge ili wawasaidie kulipa ada ile wamewekewa na ya kusafirisha miili. Jukumu letu kama Bunge linakuwa ngumu zaidi. Kwa mfano, ikiwa wikendi moja unapata wagonjwa wanne wamefariki, inakuwa pesa nyingi. Hata ukiambia jamii wachange, pia wewe kama Mbunge lazima uingie kwa mfuko ujaribu kusaidia lakini inakuwa vigumu. Kwa hivyo, mimi namuunga sana mkono Mhe. Mohamed Ali wa Nyali kwa hii Hoja aliyoleta ambayo ingekuwa imeletwa hapa zamani kujadiliwa. Ile Kamati Tekelezi ambayo inatakikana kuhakikisha kwamba mambo kama haya yanatekelezwa hapa Bungeni, ifanye hima wakati hii Hoja itakapopitishwa. Sharti ihakikishe kwamba inatekelezwa kikamilifu na wananchi wanapata afueni kuhusu masuala ya huduma ya afya katika jamii yetu. Kufikia hapo, nasema naunga mkono Hoja hii. Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi."
}