GET /api/v0.1/hansard/entries/874011/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 874011,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/874011/?format=api",
    "text_counter": 294,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Loima, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Jeremiah Lomorukai",
    "speaker": {
        "id": 13409,
        "legal_name": "Jeremiah Ekamais Lomorukai",
        "slug": "jeremiah-ekamais-lomorukai-2"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii nipate kuunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na rafiki yangu Mhe. Ali. Mahali ninakotoka kuna ufukara wa hali ya juu zaidi. Sehemu ya Loima katika kaunti ya Turkana ndiyo sehemu shida ilianzia. Kwa hivyo, wakati niliona Hoja hii, niliona kwamba watu wangu wa Loima na watu wa Kenya kijumla watafaidika zaidi. Hii ni kwa sababu ada hii itaondolewa kwa wale ambao wanakufa hospitalini. Wakati mtu ambaye hawezi kupata chakula hata mara moja kwa siku anakuwa mgonjwa, hushikwa na dukuduku hata kuenda hospitalini. Ni kwa sababu anajua hata kuingia hospitalini peke yake na kununua kile kitabu cha kuandikiwa habari anazoleta juu ya ugonjwa wake ni shida. Kwa hivyo, wakati anaamua kuenda anajua anaenda kufa. Itakuwa vizuri kama sisi Waheshimiwa ambao tunatetea haki za wale ambao walituchagua tutaunga mkono Hoja hii. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}