GET /api/v0.1/hansard/entries/874012/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 874012,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/874012/?format=api",
"text_counter": 295,
"type": "speech",
"speaker_name": "Loima, ODM",
"speaker_title": "Hon. Jeremiah Lomorukai",
"speaker": {
"id": 13409,
"legal_name": "Jeremiah Ekamais Lomorukai",
"slug": "jeremiah-ekamais-lomorukai-2"
},
"content": "Kamati husika sharti ihakikishe kwamba Hoja hii imetekelezwa. Tunajua kwamba watu wetu watafaidika pakubwa zaidi. Kule Turkana ni kama ugonjwa wa saratani ni mwingi sana katika maeneo ambayo jua ni jingi sana. Wakati mtu katika eneo hilo anapatikana na ugonjwa huo, inakuwa vigumu mtu huyo kukubali kuenda hospitalini, kwa sababu ile ada ambayo atatozwa pale ni kubwa zaidi na hataweza kuilipa. Kwa hivyo, itakuwa vizuri kama Hoja hii nzuri itapitishwa. Hasa ningependa kumpongeza Mhe. Ali. Mara nyingi amekuwa akileta Hoja ambazo zinasaidia jamii. Kwa hivyo, itakuwa vyema kama sisi Waheshimiwa tutaunga Hoja hii mkono. Ninaunga mkono."
}