GET /api/v0.1/hansard/entries/874024/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 874024,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/874024/?format=api",
    "text_counter": 307,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nakuru CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Liza Chelule",
    "speaker": {
        "id": 13126,
        "legal_name": "Liza Chelule",
        "slug": "liza-chelule"
    },
    "content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, utakubaliana nami kuwa wananchi wengine hapa Kenya wanaamua kuenda hospitali za kibinafsi na wanalipishwa pesa ambazo zinashangaza. Hawalipishi kwa mashilingi au maelfu, wanalipishwa kwa mamillioni. Mtu akikaa kwa wiki moja ama mbili, anapelekwa mbio mbio wadi ya mahututi (ICU) na analipishwa pesa nyingi. Mtu akifa anawekwa na mwili hauwachiliwi mpaka pesa zilipwe. Wananchi wa Kenya wanataabika sana. Sisi kama Bunge tuangalie mambo ya afya katika nchi yetu ya Kenya. Serikali ingekuwa na jinsi ya kuweka utaratibu wa mambo ya hospitali za kibinafsi. Kwa sababu, wanalipisha pesa nyingi sana, ilhali haijulikani wanalipisha nini. Kamati ya Afya katika Bunge hili wanapaswa kuangalia vile hizo hospitali za kibinafsi hulipisha wagonjwa. Hii ni kwa sababu Wakenya wamefinywa sana. Imefika mahali hatuwezi kunyamaza kama Wabunge. Hoja imeletwa hapa na Mbunge ambaye alifikiria vizuri na ninampongeza. Tumefurahi kama Wabunge wenzake na tumechangia. Pia, nawapongeza sana wale Wabunge ambao wameongea mbele yangu."
}