GET /api/v0.1/hansard/entries/874027/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 874027,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/874027/?format=api",
"text_counter": 310,
"type": "speech",
"speaker_name": "Tana River CWR, MCCP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Rehema Hassan",
"speaker": {
"id": 13275,
"legal_name": "Rehema Hassan",
"slug": "rehema-hassan"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi nami niweze kuchangia Hoja ya leo ambayo ni ya maana sana. Pili, nataka kumpatia shukrani kubwa sana Mhe. Mohamed Ali wa Nyali, kwa kuleta hii Hoja. Kabla sijaendelea kuchangia chochote kwanza nataka kupeana shukrani zangu za dhati kwa Gavana Joho wa Mombasa. Kwa kuwa alinisaidia wakati fulani, mmoja wa wananchi kutoka kauti yangu alikuwa amelazwa na mtoto wake, kwenye hospitali ya Coast General. Baada ya wiki mbili ule mtoto aliaga dunia na akakuwa na ada kubwa sana ya kulipa."
}