GET /api/v0.1/hansard/entries/874028/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 874028,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/874028/?format=api",
    "text_counter": 311,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Tana River CWR, MCCP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Rehema Hassan",
    "speaker": {
        "id": 13275,
        "legal_name": "Rehema Hassan",
        "slug": "rehema-hassan"
    },
    "content": "Mtoto alizuiliwa mochari, lakini nilimpigia Gavana Joho na kumwelezea hiyo shida. Kwa sababu wazazi wa yule mtoto hawana kazi, kulipa ile ada ya shilingi 300,000 ilikuwa shida sana kwao. Lakini Gavana Joho aliweza kuwasamehea hiyo ada na maiti ikatolewa na kupelekwa Tana River kuzikwa. Mungu ambariki sana, Gavana Joho. Ni wengi sana wanaopitia haya. Kando na waliofariki na wale ambao wanapitishwa kwa huduma zaidi kwenye hospitali za rufaa, kuna jambo ambalo huwa linaniumiza roho yangu. Kuna wale wagonjwa ambao wanafanyiwa dialysis, ambapo utapata kila wiki mtu anatakikana asafishwe. Utapata pengine kama ni hospitali ya serikali, mtu analipa shilingi 15,000 kila wiki na hana uhakika ile hali yake itarudi kawaida lini. Ningependa Serikali ishughulikie jambo hili. Mhe. Mohamed anapaswa kuweka kipengele kidogo kwa sababu wale wanafanyiwa dialysis wanaumia sana, maanake wanalipa kila wiki. Pia, siku hizi ajira hakuna. Hali ya anga ni vile mnavyoona. Siku hizi hakuna mvua kama zamani. Yule mkulima anayetegemea kupata mmea ili aweze kujikimu kimaisha siku hizi imekuwa ni shida. Hata chakula hawapati. Magonjwa yamekuwa mengi sana, ya saratani,"
}