GET /api/v0.1/hansard/entries/874031/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 874031,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/874031/?format=api",
    "text_counter": 314,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Tana River CWR, MCCP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Rehema Hassan",
    "speaker": {
        "id": 13275,
        "legal_name": "Rehema Hassan",
        "slug": "rehema-hassan"
    },
    "content": "alivyozungumza Mhe. Chelule kuwa hospitali za kibinafsi ziweze kuwa na njia ya kuangaliwa vile zinalipisha wananchi kwa sababu ile yao huwa si huduma wanapatiana lakini ni biashara. Mtu amekimbilia pale, si kwa kupenda bali kuwa apate huduma na aweze kupona na kuendelea na maisha. Wakati unaenda pale, jambo la kwanza kumwona daktari peke yake ile ada anaitisha ni kama shilingi elfu tano ama 10. Hujaenda hata kuangaliwa ni ugonjwa upi uko nao. Akishamaliza kabla mtu apatiwe matibabu, anambiwa ni lazima uweke kiwango fulani cha pesa ndiyo uweze kuhudumiwa. Huyo mtu maskini anaenda pale ni mgonjwa na hana pesa halafu unamwambia alipe Sh50,000 ndio aanze kuhudumiwa. Yule mtu hatapata matibabu au huduma. Kwa hivyo, ninasisitiza kwamba Kamati ya Afya ikae chini ijaribu kuweka njia ya kuhakikisha watu hawa hawaitishwi pesa zaidi ili angalau wakikimbilia kwa hospitali za kibinafsi waweze kusaidika. Pia, wazidi kuongeza huduma katika hospitali za serikali. Pia napenda kusema kuwa serikali za kaunti zijaribu kuangalia maslahi ya wahudumu wa hospitali ili warudi kazini wawahudumie wananchi. Wanapovutana nao, wanaoumia ni wananchi walioko hospitalini. Kama mlikuwa mmekubaliana mtawalipa pesa zao, tafadhali walipeni warudi hospitalini wananchi wapate huduma. Nikimalizia, nataka kutoa shukrani tena kwa Mhe. Mohamed na naunga mkono Hoja hii. Asante."
}