GET /api/v0.1/hansard/entries/875482/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 875482,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/875482/?format=api",
    "text_counter": 226,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taveta, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Dr.) Naomi Shaban",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Nampongeza mwenyekiti kwa kazi nzuri ambayo amefanya kwenye Taarifa hii. Tangu hazina hiyo ianzishwe, kamati iliyowekwa na Bunge la 12 ni muhimu. Lakini juu ya hapo, ningetaka kutoa taarifa kwamba kuna umuhimu wa Serikali kuu kutengeneza jinsi hazina hiyo itaweza kuangalia maeneo yote ya Bunge hapa nchini. Kama unavyofahamu, maeneo ni 290 na sio rahisi kwa kila mtu kwenda kila mahali wakati wowote. Pesa za ugatuzi zingelifuata namna pesa hizi za hazina za maeneo Bunge zinavyotumika, bila shaka tungeona faida yake. Pesa za ugatuzi zimekuwa zikifujwa na huu ulikuwa mfano wa kugatua pesa kutoka Serikali kuu kushuka nchini lakini sasa hivi tunaona kuwa ni malalamishi kila pahali tunapopita. Sina mengi ya kusema isipokuwa tuzidi kuangalia jinsi tutakavyoboresha matumizi ya pesa hizi na kuweza kusimamia na kuhakikisha kuwa pesa hizo zinatumika vile ambavyo ilivyotengwa kwa mujibu wa sheria ya pesa za hazina za mashinani. Naunga mkono taarifa hii."
}