GET /api/v0.1/hansard/entries/875604/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 875604,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/875604/?format=api",
"text_counter": 348,
"type": "speech",
"speaker_name": "Bahati, JP",
"speaker_title": "Hon. Onesmas Ngunjiri",
"speaker": {
"id": 1179,
"legal_name": "Onesmas Kimani Ngunjiri",
"slug": "onesmas-kimani-ngunjiri"
},
"content": "Kazi ya Wabunge ni mambo mawili: Kuangalia usalama na elimu. Mambo haya yasiwe yakusukumia Wabunge ili waonekane hawafanyi kazi. Kwanza, tukirudi kwa hospitali, ni lazima tuchunge mambo ya Serikali kuu. Serikali kuu imesema kuwa maternity, nursery, primary na elimu ya secondary itakuwa ya bure na ukiingia university unapewa pesa. Sasa kazi ya mzazi itakuwa ni nini? Board ya shule haiwezi kusema kuwa hata choo ikianguka na NG-CDF haina pesa, haiwezi kuwaambia wazazi wachange pesa kwa sababu wameambiwa elimu ni ya bure. Kwani mtoto ni wa Serikali? Mzazi pia ana jukumu la kuangalia mambo nyeti katika shule ili asaidie. Lakini tumeweka ugonjwa wa kusema kila kitu ni bure. Kwa kweli, hakuna kitu cha bure. Wanasema maternity ni bure lakini juzi tumeona mtu akimtoa mtoto wake kwa Hospitali ya Kenyatta kwa siri kwa kukosa kulipa ada ya hospitali. Kama maternity ni ya bure, kwa nini huyo mtu alienda kumtoa mtoto wake kwa hospitali kama amejificha? Si ukweli eti kila kitu ni cha bure. Mtoto hawezi kuwa darasani bila kuchanga pesa yoyote."
}