GET /api/v0.1/hansard/entries/875606/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 875606,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/875606/?format=api",
    "text_counter": 350,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Bahati, JP",
    "speaker_title": "Hon. Onesmas Ngunjiri",
    "speaker": {
        "id": 1179,
        "legal_name": "Onesmas Kimani Ngunjiri",
        "slug": "onesmas-kimani-ngunjiri"
    },
    "content": "Kuma mambo ambayo tunahitaji kuangalia na kuiambia Serikali kuu ili wakisema kitu, wawahusishe Wabunge. Wabunge wako na mzigo mkubwa sana. Ni muhimu kwa kila mtoto kuenda shule lakini ukiangalia mikakati ambayo imewekwa, hairuhusu kila mtoto kuwa shuleni. Hakuna madarasa, mijengo na barabara za kuingia shuleni. Kwa hivyo, kuna mambo nyeti mengi. Pia, naunga mkono mazungumzo haya ya NG-CDF kwa sababu inasaidia sana. Nakubaliana na ndugu yangu, Mhe. Sankok. Katika eneo Bunge langu, ninajenga madarasa kama vile alivyosema, nikitumia Kshs800,000. Haya madarasa yako na tiles, key, ceiling na kila kitu. Nitaongeza iwe Kshs1 milioni ili nikipatiana darasa liwe na kila kitu. Hii ni kwa sababu unapata hakuna viti na wazazi hawawezi kuitishwa pesa za viti. Kwa hivyo, inabidi tuongeze pesa kutoka kwa NG-CDF. Wakati huu, tunazungumzia Bajeti ambayo inakuja. Bajeti tuliyopitisha tumebakisha miezi minne ili tupitishe nyingine na hizo pesa mpaka sasa hazijatoka. Unapata watoto wanasukumwa huko kwa sababu pesa hazijatoka. Tukipitisha Bajeti inayokuja, itakuwa ya mwaka mwingine na itapitana na ya mwaka jana kama pesa hazitatoka. Hili ni jambo nyeti. Serikali inapaswa kuangalia mambo gani yanapaswa kupewa kipao mbele ili Mbunge aweze kusaidia. Kwa mfano, ukiangalia katika maeneo bunge, Wabunge wamefanya kila kitu. Wamejenga madarasa, laboratories na kila kitu kinaendelea. Ukienda kwa magavana, wanatumia Kshs1.5 milion kujenga darasa moja na hata hilo darasa likitingizwa na upepo, litaanguka. Sitaki kuwatetea MCAs, lakini nataka kusema kuwa wangepewa pesa kama Wabunge kwa sababu sisi tuko hapo kwa sababu ya public participation, lakini pesa iko na fundmanager na accountant . Hata kama tunataka kuwasaidia MCAs, kuna constituency na wardadministrator s ambao hatujui wanafanya nini. Wanapaswa kupatiwa hizo pesa ili MCAs wawe"
}