GET /api/v0.1/hansard/entries/875609/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 875609,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/875609/?format=api",
"text_counter": 353,
"type": "speech",
"speaker_name": "Bahati, JP",
"speaker_title": "Hon. Onesmas Ngunjiri",
"speaker": {
"id": 1179,
"legal_name": "Onesmas Kimani Ngunjiri",
"slug": "onesmas-kimani-ngunjiri"
},
"content": "Lakini pesa inatumiwa huko juu, inakuliwa na kuibiwa na MCAs wanabebeshwa mzigo kwa sababu hawana kitu cha kuonyesha kazi ambayo wamefanya. Nimesikia kutoka kwa Wabunge wengi kuwa mwelekeo na maoni yao ni kurekebisha mambo yanayosumbua. Wabunge wanafaa kuongea ukweli. Unajua hii mambo ya handshake tulifikiria watawatetea wananchi kwa sababu wako minority . I am happy, I can see what the party and the Opposition are doing. Theyare still playing their role kusaidia kupigania haki. Ningetaka kusema kuwa nchi hii kama haina minority ni majority pekee, pesa za umma zitaibiwa na kila kitu kitakwisha. Ninafurahi kwa kazi ambayo wanafanya kutetea mambo mabaya ambayo Serikali inaweza kufanya. Nimeona ndani ya Bunge hili tuko pamoja. Wakati mwingine, tulikuwa tunapigana kisiasi lakini jukumu letu sisi wote ni kutetea mwananchi na kusikizana kwa mambo yaliyo mbele yetu. Hakuna Mbunge wa minority au majority. Kazi yetu na shida zetu zote ni sawa. Nashukuru wale Wabunge ambao wameunga mkono jambo hili ili turekebisha mambo ambayo tunaona yatatusumbua ili tufikishe maendeleo mashinani. Lakini Serikali kuu haipaswi kusema kila kitu ni cha bure kwa sababu italeta shida. Hata mama akijaribu kusema jambo fulani, mzee anasema kila kitu ni cha bure na kwa hivyo, waendelee. Tukiendelea hivyo bila mpango, tutakuwa na shida ya kuzaliwa kwa watoto wengi. Kwa hayo machache, nashukuru."
}