GET /api/v0.1/hansard/entries/875809/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 875809,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/875809/?format=api",
"text_counter": 132,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "KWAMBA, tukitambua kuwa Ibara ya 43 ya Katiba imebainisha kuwa kila mtu ana haki ya kupata kiwango bora zaidi cha afya, kinachojumuisha haki ya kupata matunzo ya kiafya na kutonyimwa matibabu ya dharura; aidha, ikifahamika kwamba gharama za matunzo ya kitabibu katika taasisi za kiafya za kibinafsi zingali ghali mno, hivyo kuwalazimu Wakenya wengi kupendelea kusaka huduma hizo kwa hospitali za umma; tukizingatia kwamba, licha ya bei nafuu ya matibabu katika hospitali za umma ikilinganishwa na hospitali za kibinafsi, bado Wakenya wengi hawamudu, hivyo basi kutumbukia kwenye madeni, ufukara na dhiki wanaposhindwa kulipa malimbikizi ya gharama za matibabu yao na ya wapendwa wao; Bunge hili linahimiza Serikali ya kitaifa kufutilia mbali gharama zote za matibabu ya wagonjwa wote wanaofariki wakipokea matibabu katika hospitali za umma za rufaa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}