GET /api/v0.1/hansard/entries/875829/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 875829,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/875829/?format=api",
"text_counter": 152,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nyali, Independent",
"speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
"speaker": {
"id": 13455,
"legal_name": "Mohammed Ali Mohamed",
"slug": "mohamed-ali-mohamed"
},
"content": " Mheshimiwa Naibu Spika, kuweka wazi wacha tuseme “iwapo Bunge hili litapitisha Hoja hii ambayo tulileta wiki iliyopita”. Kwa ufupi, Hoja hii itasaidia mwananchi wa kawaida katika masuala ya gharama ya maisha kwa sababu sisi Wabunge hatuna mamlaka dhidi ya mambo fulani yanayotendeka katika taifa hili. Kwa mfano, swala la afya liko katika ugatuzi. Ni swala ambalo wahusika wakuu katika kaunti ni magavana ambao wanafaa wasaidie katika mambo haya lakini sio wote. Wengine wamezembea katika majukumu yao, hivyo basi kutuletea kazi kubwa zaidi. Wiki iliyopita sikuweza kugusia mambo mawili. Katika Hospitali ya Kitaifa ya Rufaa ya Kenyatta, kila wadi ina vitanda vinne. Kwa ujumla, hospitali iko na wadi kama 50. Asilimia 78 ya Wakenya hawawezi kulipa kwa sababu katika wadi hizi utapata watu wanalazwa chini, hawapati dawa na kuna uhaba wa madaktari. Kwa hivyo, chanzo kubwa kabisa kinachosababisha vifo ni uzembe katika Serikali kuboresha sekta ya afya. Kwa mfano, Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta pekee inapoteza Kshs600,000 kwa siku kwa watu wasioweza kulipa kwa sababu ya maradhi kama vile saratani au figo."
}