GET /api/v0.1/hansard/entries/875834/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 875834,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/875834/?format=api",
    "text_counter": 157,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nyali, Independent",
    "speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
    "speaker": {
        "id": 13455,
        "legal_name": "Mohammed Ali Mohamed",
        "slug": "mohamed-ali-mohamed"
    },
    "content": " Shukrani, Mhe. Naibu Spika. Katika mradi wa Linda Mama, Serikali inalipa Kshs17,000 lakini hii haimudu kujifungua kwa upasuaji ambao kwa lugha ya kimombo ni Caesarean Section . Je, hatima ya mwanamke anayejifungua kwa upasuaji iko vipi? Je, hatima ya mtoto ambaye anazaliwa kabla ya siku yake iko vipi? Hivi ndivyo vipengele ambavyo tunaangalia kwa undani na kuhakikisha ya kwamba mwananchi wa kawaida amesaidika. Tutahesabu watu na tutatumia Kshs6 bilioni. Pia, kuna kauli mbiu ya kura ya maoni ambapo zaidi ya Ksh18 bilioni itatumika. Hizi pesa zitatumika kwa mambo ambayo hayana uzito kwa mwananchi wa kawaida. Badala hizi pesa zitumike katika afya na ujenzi wa taifa hili, zinatumika katika masuala ambayo hayasaidii asimilia kubwa ya Wakenya, asilimia 80 ambao ni maskini."
}