GET /api/v0.1/hansard/entries/875976/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 875976,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/875976/?format=api",
"text_counter": 299,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": " Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuungana na wenzangu katika kuwapongeza wanakamati kwa kazi yao nzuri ambayo wamefanya kuhusiana na Ripoti hii ambayo imeletwa Bungeni. Kwa kweli, wengi wamechangia kuhusiana na masuala haya, na haswa kuhusu pesa za NG-CDF – Hazina ambayo imekuwepo kuanzia mwaka wa 2003. Ni vyema Wakenya wafahamu utaratibu wa NG-CDF na mabadiliko ambayo yamefanyika katika NG-CDF. Ukweli ni kwamba fedha hizi, kuanzia mwaka wa 2003, zimeleta mabadiliko makubwa nchini Kenya. Leo kuna mengi yanayozungumziwa kuhusiana na maendeleo na mengineo lakini, ukweli ni kwamba, fedha hizi zimeonekana katika sehemu za mashinani. Fedha hizi zimeleta maendeleo makubwa katika maeneo Bunge. Faida ambayo imepatikana kutokana na matumizi ya NG-CDF ni nyingi sana ukilinganisha na hazina nyingine zilizoanzishwa na Serikali ya Kitaifa na serikali za kaunti. Hizi sitaki ziwe ni sifa ambazo twajipa sisi Wabunge. Ni lazima Wakenya wafahamu kwamba sisi kama Wabunge, hatuhusiki kwa namna yoyote kwenye utendakazi wa NG-CDF. Fedha hizi zimeweza kutumika kwa mipangilio yake na Wakenya wanaziona. Huu ni ushahidi kamili."
}