GET /api/v0.1/hansard/entries/875977/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 875977,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/875977/?format=api",
    "text_counter": 300,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Tatizo ambalo bado lipo mpaka sasa ni kwamba Wakenya bado wanahitaji maendeleo. Changamoto ni nyingi. Ni lazima Serikali ifahamu kikamilifu. Miongoni mwa mbinu zilizotumika kugawanya fedha hizi katika maeneo Bunge hapo ni idadi ya watu na hali ya umaskini katika sehemu hizo. Utakubaliana nami kwamba baadaye, mbinu hiyo ilibadilishwa na kila eneo Bunge likawa linapokea kiwango sawia cha fedha kutoka NG-CDF. Hakuna eneo Bunge linalopata pesa nyingi kuliko lingine. Ukweli ni kwamba maeneo Bunge hayafanani. Kuna sehemu ambazo zimeendelea na kuna sehemu ambazo bado kuna udhaifu na umasikini mkubwa. Mbali na kusema kwamba tuangalie idadi ya watu, sidhani ni kiegezo kizuri kwa sababu utapata idadi ya watu ni ndogo lakini matatizo na umaskini ni mwingi. Kwa hivyo, naunga mkono lile pendekezo au mwongozo wa kila eneo Bunge lipewe fedha zile. Ukweli ni kwamba fedha hizi zinazopelekwa kwa maeneo Bunge, ni fedha ambazo zinahitajika. Naunga mkono waheshimiwa ambao wamechangia swala hili. Wanahitaji kuongezeka. Kuna uwezo na njia za kuongeza fedha hizi. Kwa mfano, fedha hizi zimewekewa mipangilio ya kwamba zitatumika katika maswala ya elimu ama ulinzi. Utapata kuwa katika Serikali ya Kitaifa, kuna pesa ambazo zinatengwa kupewa wizara inayohusika na maswala ya elimu ama ulinzi, wakati The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}