GET /api/v0.1/hansard/entries/875978/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 875978,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/875978/?format=api",
    "text_counter": 301,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Bajeti ya Kenya inapangwa. Ni kama kusema kuwa fedha hizi zinazopelekwa katika Wizara ya Elimu, matumizi yake ni yale ambayo yamepangiwa miongoni mwa matumizi ya NG-CDF. Kwa maoni yangu, ningesema kwamba, Serikali izingatie pakubwa. Ni kama kutumia pesa kwa njia moja. Leo utapata kwamba, eneo Bunge linahitaji kujengewa madarasa. Baada ya pesa zile kupatiwa NG-CDF, zingine zinapatiwa wizara katika kuifanya kazi hiyo hiyo. Fedha hizi mwishowe hazionekani dhamani yake katika wizara hizi. Kila mmoja wa Wabunge hawa anaweza kutoa ushahidi mkubwa kuwa zile pesa tunazoziona ni zile zinazotumika kwa NG-CDF. Zile ambazo zinaenda katika wizara halafu wizara inapendekeza kuwa kujengwe madarasa, hatuelewi zinagawanywa vipi."
}