GET /api/v0.1/hansard/entries/875979/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 875979,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/875979/?format=api",
    "text_counter": 302,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Ni lazima tuzingatie haya pakubwa. Nchi yetu iko na malengo na maono katika kuendeleza elimu, lakini changamoto ni nyingi. Sisi Wabunge ndio ambao tunapambana na changamoto hizi katika maeneo Bunge yetu mashinani. Serikali imepanga kwamba watoto wasome bure na madarasa yajengwe. Lakini utapata kwamba mipangilio hii Serikali imependekeza haijakamilika. Utapata kwamba katika shule moja, darasa moja lina watoto kati ya mia moja na mia mbili kwa sababu elimu ni bure. Hii ni hali ya kusikitisha. Ingekua ni vyema kwamba, kabla hawajakuja na mipangilio hii, wangefanya utafiti kikamilifu katika maeneo Bunge yote katika kaunti zote na kujua yale yanayohitajika kukamilishwa au kutekelezwa kwa mapendekezo yao ya watoto kusoma bure."
}