GET /api/v0.1/hansard/entries/875980/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 875980,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/875980/?format=api",
    "text_counter": 303,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Swala la kutaka kufanya mambo na wakenya halafu baadaye kuona wanadanganywa, sioni kama yatatatua matatizo yetu. Kuna dharura kubwa ya Serikali kuzingatia. Ndio kwa sababu tunataka wanafunzi au watoto wetu wa kila sehemu waende shule. Tunataka wazazi wasaidiwe mizigo ya kulipa karo shuleni. Ningependa kuambia Bunge hili kwamba, hadi tunavyozungumza hivi sasa, mipangilio hii haijaweza kuwa na mwongozo kikamilifu kwa sababu matatizo mengi hayajaweza kusuluhika. Ningependekeza kama wenzangu walivyotoa maoni kuhusu fedha za NG-CDF. Nina imani kwamba utafiti huu umefanyika na umeonekana kuleta mabadiliko makubwa. Fedha hizo ziongezwe katika kuendesha maswala haya ya maendeleo katika maeneo Bunge yote ya Kenya hii ili tuweze kuhakikisha kuwa matatizo ya jamii katika swala nzima la elimu na mengineyo yamesuluhishwa."
}