GET /api/v0.1/hansard/entries/87746/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 87746,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/87746/?format=api",
"text_counter": 155,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mungatana",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 185,
"legal_name": "Danson Buya Mungatana",
"slug": "danson-mungatana"
},
"content": "Bw. Spika, Waziri Msaidizi bado hajalijibu Swali hili kikamilifu. Kila Serikali ambayo imewahi kutafuta kura katika sehemu ya Pwani, imeahidi kuijenga barabara hiyo. Hivi sasa, viongozi kutoka pande zote mbili zilizokuwa zikipigania urais wako Serikalini. Sisi tunazungumza kwa niaba ya wananchi wa Taveta. Tungependa Waziri Msaidizi aseme ni lini ujenzi wa barabara hiyo utaanza ili iwekwe lami. Tafadhali, Bw. Spika, kama Waziri Msaidizi hana jibu, ni afadhali kujibiwa kwa Swali hili kuahirishwe ili arudi hapa juma lijalo na atuambie ni lini barabara hiyo itaanza kufanyiwa kazi. Kwa hivyo, tunaomba Swali hili liletwe juma lijalo ili Waziri Msaidizi aweze kuleta jibu na kusema ni lini ujenzi wa barabara hiyo utaanza. Stori nyingi wananchi wamechoka nazo. Hawataki stori nyingi!"
}