GET /api/v0.1/hansard/entries/877738/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 877738,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/877738/?format=api",
"text_counter": 179,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, mambo kama haya yanaendelea kutokea katika sehemu tofauti. Ukiangalia hata hapa Nairobi, watoto wengi ambao wanarandaranda wanachukuliwa kama wahalifu, ilhali ni jukumu la Serikali ya Kaunti kuhakikisha kwamba wanapata makao, chakula na nguo, ili waishi kama binadamu wengine. Jambo kama hili ni lazima lichunguzwe na tuhakikishe kwamba wale ambao walihusika na huu unyama wanapewa adhabu ya kutosha. Asante, Bw. Naibu Spika."
}