GET /api/v0.1/hansard/entries/878019/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 878019,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/878019/?format=api",
"text_counter": 460,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Ripoti ya Kamati kuhusu shida zinazowakumba wakulima wa mahindi. Kwanza, ninapongeza Kamati iliyoongozwa na Seneta (Prof.) Kamar na Seneta Wetangula kwa kazi nzuri iliyoifanya kuhakikisha kwamba dhambi zote ambazo wakulima wa mahindi walitendea katika eneo la kasikazini ya ponde la ufa na kwingineko nchini Kenya yameaangaliwa na kutolewa suluhisho. Hii Ripoti ya mahindi inatukumbusha mambo ya sukari katika eneo la pwani. Kiwanda cha Sukari cha Ramisi kilikuwa kiwanda cha kwanza kusaga sukari katika miaka ya 1950. Jambo la kusikitisha ni kwamba sukari ililetwa kwa wingi kama yalivyoletwa mahindi mwaka jana na kiwanda kile hakingeweza kusaga sukari kwa sababu soko ilikuwa imejaa sukari kutoka nje. Jambo hili lilifanya kiwanda hicho kufungwa Jambo la kufurahisha ni kwamba mtambo mwingine umefunguliwa katika eneo la Ramisi na unasaga sukari katika mashamba yale yale ambayo wakulima wa Pwani walikuwanayo. Tumeona pia wakulima wa korosho walilia kama wanavyolia wakulima wa mahindi. Mpaka sasa, hakujakuwa na suluhisho. Mtambo wao wakorosho pia ulinunuliwa na mtu binafsi. Kwa hivyo, matatizo yalitokea kwa sababu, kwanza, kuna upungufu katika Serikali. Haina mipango yoyote kuhusiana na mazao ambayo yanatolewa katika nchi yetu. Haina mipango yoyote ya soko na jinsi ya kuthibiti mazao yale ili kuhakikisha kwamba mwananchi hapati hasara. Bw. Naibu Spika, tumeona pia kwamba vikundi ambavyo vinajihusisha katika mambo ya ufisadi vinapata fursa kwa sababu Serikali imelemaa katika kuangazia maswala ya wakulima, yakiwemo kutafuta soko la mazao yao. Bei ya mbegu na mbolea iko juu. Ni vizuri tuhakikishe wakulima wanapata pembejeo mapema ili waweze kuzalisha mazao yao kwa njia ambayo ni rahisi. Kupitia upungufu huo, vikao vya ufisadi vinapata fursa ya kujitajirisha kibinafsi katika nchi hii, wakati wakulima wanaendelea kupata shida. Bw. Naibu Spika, Ripoti hii inazungumzia mahindi ghushi ambayo yaliuziwa NCPB na watu wakalipwa pesa ilhali hawakupeleka mahindi yoyote. Katika Ripoti hii, kuna mahindi ambayo yaliuzwa ilhali tayari yalikuwa yameharibika na hayakuwa salama kwa matumizi ya binadamu au Wanyama. Kwa hivyo, tunafaa kuunga mkono Ripoti hii na kuhakikisha kwamba yale ambayo yamependekezwa kufanyika, yanafanyika ili wakulima wasiendelee kuteseka katika nchi yetu. Bw. Naibu Spika, wakulima wengi si maskini, lakini kutokana na ukosefu wa soko na pembejeo kupeanwa mapema, imewafanya watu wa kuombaomba kila mwaka. Leo wanaomba mbolea, kesho soko na kesho kutwa vitu vingine. Watoto wao wanashindwa kwenda shule na kumaliza Masomo kwa sababu Wazazi hawana pesa. Wangekuwa na pesa wangeweza kusomesha watoto wao bila matatizo. Bw. Naibu Spika, tumeona pia kwamba ijapokuwa ukulima umegatuliwa, serikali zetu za kaunti zimetenga bajeti ndogo sana kuangazia ukulima. Kwa hivyo, kama Seneti, tunafaa kuhakikisha kwamba zile bajeti zinazotengenezwa katika kaunti zetu The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}