GET /api/v0.1/hansard/entries/880042/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 880042,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/880042/?format=api",
"text_counter": 310,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda. Ningependa kuungana na wenzangu kuunga mkono marekebisho haya ya Mswada huu kuhusu serikali za kaunti. Tunapaswa kama Wakenya kujipongeza wenyewe na kuipongeza nchi hii kwa Katiba tuliyopitisha kuhusiana na mambo mengi, mojawapo ikiwa suala la serikali za kaunti. Leo marekebisho tunayofanya hapa ni kutokana na hofu kubwa kuwa serikali za kaunti kuonekana namna zitakavyojiendeleza na namna zitakavyodumu katika kuendeleza mambo yao. Ndiposa mwongozo huu tuko nao leo waonyesha hofu iliyokuwapo ni kwamba serikali 47 za kaunti huenda zizifanye vyema ama kutokuwa na usawa. Ndiyo sababu kukawekwa mikakati kama hii ili mambo haya yatakapojitokeza ifahamike ni vipi yatarekebishwa. Ukweli ni kwamba, ningependa kuzipongeza serikali za kaunti takriban zote. Kutoka zianze masuala haya hakuna kaunti imepitia changamoto hizi isipokuwa tu kaunti moja. Imetajwa na wenzangu hapa lakini vile vile, haikufika kiwango cha hofu iliyokuwepo kwa Wakenya wakati walipokuwa wakipanga Katiba hii. Lazima tukubali pakubwa fikra ya kuwa na serikali za kaunti imechangia pakubwa maendeleo ya nchi hii. Tumeshuhudia mambo mengi yamebadilika na maendeleo yamekuwapo katika sehemu mbali mbali katika nchi hii. Ingawaje hakuna jambo ambalo halina changamoto, lakini ukweli ni kwamba tunashukuru Mwenyezi Mungu kutokana na serikali za kaunti kuonyesha mabadiliko makubwa. Kumekuwa na tofauti kubwa katika nyanja tofauti tofauti. Ingawaje, ni vizuri kuendelea kuhakikisha kwamba zimepigwa darubini ama kuhakikisha kwamba zitadumu na kufuata sheria na utaratibu unaotakikana. Naunga mkono Mswada huu nikiamini pakubwa haya yote ambayo tumeyaweka wazi hapa yatakuwa ndio mwongozo na uangalifu wa serikali za kaunti. Tuhakikishe kwamba The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}