GET /api/v0.1/hansard/entries/880553/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 880553,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/880553/?format=api",
    "text_counter": 490,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": " Asante Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Ningependa kwanza kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa fursa hii ya kuchangia Ripoti hii ambayo tunayo hapa Bungeni. Mimi ni Mwanakamati wa Kamati ya Hazina ya Maendeleo ya Maeneo Bunge. Vile vile, ningependa kumshukuru Mwenyekiti kwa kuileta Ripoti hii. Waheshimiwa wamezungumzia masuala ya Kamati ya Hazina ya Maendeleo ya Maeneo Bunge. Vile vile, ningependa kumpongeza Mheshimiwa Angwenyi kwa kuelezea historia fupi ya namna Hazina hiyo ilivyoanza. Ni takriban miaka 15 tangu Hazina hiyo ianzishwe. Ukweli ni kwamba Wakenya wengi wameiona faida ya Hazina hiyo tangu ianze hadi sasa inavyoendelea. Wengi waliochangia wamezungumzia changamoto nyingi ambazo ziko bali ya kwamba kuna faida nyingi ambazo zimepatikana katika maeneo Bunge tofauti tofauti. Ukweli ni kwamba faida nyingi zimepatikana. Sisi ni Wabunge ambao tumewajibika kuyatekeleza majukumu yetu katika fedha hizi. Watu wengi wanaziangalia kama fedha zinazosimamiwa na Wabunge mashinani. Wananchi huuliza hizi fedha kupitia kwa Wabunge."
}