GET /api/v0.1/hansard/entries/880554/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 880554,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/880554/?format=api",
    "text_counter": 491,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Ni jambo la kusikitisha kuona pakubwa kwamba hali hii bado inaendelea katika nchi yetu. Utakubaliana na mimi ya kwamba Constituencies Development Fund (CDF) ilibadilishwa jina kuongezwa jina kwamba ni pesa za Serikali kuu kutokana na mipangilio ya Serikali ya ugatuzi. Hapo awali CDF ilikuwa na changamoto baada ya Wakenya kupitisha Katiba. Walisema ya kwamba CDF hairuhusiwi kuwepo tena kwa sababu ya ugatuzi. Katika historia fupi, baada ya hapo, masuala haya yalifika mpaka mahakamani na ikabadilishwa jina kuongezwa kwamba ni fedha za Serikali ya kitaifa. Waheshimiwa wengi ambao wamechangia leo wanalalamika kwamba hizi fedha ni kidogo kwa sababu majukumu na matakwa ni mengi katika maeneo Bunge. Suala hili lisiendelee kuchangiwa na Waheshimwa kwa sababu suluhisho lipo. Hazina ya NG-CDF ilipangiwa kuangalia masuala ya elimu na usalama."
}