GET /api/v0.1/hansard/entries/880555/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 880555,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/880555/?format=api",
"text_counter": 492,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Vile vile, katika Bajeti ya nchi hii wakati pesa hizi zinavyogawanywa, fedha nyingi zinapelekwa katika wizara zinazohusika na elimu na usalama. Tukienda mashinani kama Waheshimiwa, tunaulizwa na wananchi masuala ya elimu na usalama. Wananchi wanatarajia pesa za NG-CDF zisimamie usalama na elimu. Nina swali kwa Serikali ya kitaifa. Kwa nini inapeana pesa nyingi kwa Wizara ya Elimu na kuna majukumu ambayo wamepeana kusimamiwa na NG-CDF katika masuala ya elimu? Maoni yangu katika jambo hili ni kuwa wakati Bajeti ya nchi hii inapopangwa, asilimia kubwa ya fedha ambazo zinaenda kwa Wizara ya Elimu ziletwe katika kuimarisha NG-CDF. Katika neno “NG-CDF”, kuna fedha ambazo zinaenda kwa wizara katika maendeleo ya elimu. Pia, kuna neno “ National Government .” Kwa hivyo, hii ni pesa ya Serikali lakini si pesa ya Wabunge. Kwa hivyo, pesa zinapelekwa kwa wizara lakini majukumu yako kwa NG-CDF. Waheshimiwa wanaangalie masuala ya elimu kupitia kwa NG-CDF. Ninaona hili ni jambo ambalo linahitaji kuangaliwa vizuri."
}