GET /api/v0.1/hansard/entries/880559/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 880559,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/880559/?format=api",
"text_counter": 496,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Kuna changamoto ambazo tunapata kama Kamati katika suala la kuridhisha haya mambo kwa sababu Wabunge wanalalamika. Tuko mwezi wa tatu na utapata ya kwamba maeneo Bunge hayajapata kabisa ule mgao wa NG-CDF wa mwaka huu. Wengine wamepata kama Ksh10 milioni. Wabunge wenzangu wanalalamikia Kamati ya NG-CDF. Ukweli ni kwamba sisi kama Kamati, tunajitahidi vilivyo kuhakikisha kwamba Wabunge wamepata pesa kwa sababu tunaelewa hali hii. Matatizo yako katika Wizara ya Fedha katika kutoa pesa hizi. Ningewaambia Wabunge wenzangu kwamba tunajitahidi kuhakikisha tumefuatilia jambo hili kwa sababu tunajua zile changamoto Wabunge wanapitia katika maeneo Bunge yao. Wizara ya Fedha haijatilia maanani kuhakikisha kwamba wakati mwafaka ukifika, hizi fedha za NG-CDF zinafika kwa wahusika kwa wakati wake na kwa namna inavyotakikana."
}