GET /api/v0.1/hansard/entries/880560/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 880560,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/880560/?format=api",
    "text_counter": 497,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Ningependa kusema ya kwamba hapo awali, mgao wa NG-CDF ulikuwa unaangazia masuala ya umaskini na wingi wa watu katika sehemu. Waheshimiwa wanalalamika kuhusu suala hili. Tutafute njia ya kuhakikisha kwamba kuna sehemu ambazo zinahitaji hizi fedha zaidi kuliko sehemu zingine. Ninaunga mkono jambo hili, lakini ifahamike pakubwa kwamba kuna miegezo mingine ambayo tunafaa kuangalia. Kwa mfano, idadi ya watu siyo suala la kuzingatiwa kikamilifu. Suala la kuzingatiwa kikamilifu ni umaskini. Unaweza kupata idadi ya watu katika sehemu ni kidogo lakini umaskini ni mkubwa sana. Kwa hivyo, tuwe waangalifu kama Waheshimiwa katika kutaka kurekebisha haya mambo tusije tukadhulumu sehemu zingine na wengine tukawapa mwongozo na kuwainua."
}